Friday, October 21, 2016

HEKIMA



Bwana & Neno lake Je Mwongozo Us / The Lord His Word Will Guide Us
  • Zaburi 5:8 - Bwana, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uisawazishe njia yako mbele ya uso wangu,
  • Zaburi 25:4, 5 - Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.
  • Zaburi 25:9 -Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.
  • Zaburi 27:11 -Ee Bwana, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
  • Zaburi 32:8 - Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
  • Zaburi 37:23 - Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake.
  • Zaburi 73:24 - Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
  • Zaburi 119:18 - Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.
  • Zaburi 119 :105 - Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
  • Zaburi 119:130 - Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
  • Zaburi 143:8 - Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.
  • Mithali 3:5, 6 - Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
  • Mithali 6:22 - Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.
  • Isaya 30:21 - Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
  • Isaya 42:16 - Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.
  • Isaya 50:4 - Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
  • Isaya 58:11 - Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
  • Yeremia 10:23 - Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.
  • Yeremia 31:9B - Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
  • 2 Wakorintho 5:7 - (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
  • Waebrania 4:12 - Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Bwana Je Tupe hekima / The Lord Will Give Us Wisdom


  • 2 Mambo ya Nyakati 19: 6B - Akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu.
  • Mithali 2:3, 5, 6 - Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
  • Mithali 16:1 - Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.
  • Mithali 28:5 - Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote.
  • Isaya 11:2 , 3 - Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
  • Danieli 1:17 - Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieliii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
  • Yakobo 1:5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
  • Zaburi 143:8 - Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.
  • Zaburi 143:10 , 11A - Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;



Hekima katika shauri Kiungu / Wisdom In Godly Counsel

  • Mithali 1:5 - Mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
  • Mithali 12:15B -Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
  • Mithali 15:22 - Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.
  • Mithali 19:20 - Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.
  • Mithali 20:18 - Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.
  • Mithali 24:6 - Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
  • Yohana 7:24 - Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
  • Yakobo 3:17 - Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
  • 2 Wakorintho 13:1B - Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.

No comments:

Post a Comment