Monday, October 10, 2016

MISTARI KWENYE BIBLIA KUHUSU MAOMBI.

TUMIA VIPENGELE HIVI VITAKUSAIDIA KATIKA KUKUA KIROHO KATIKA SWALA LA MAOMBI.



  • Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; Mathayo 7:7
  • Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. - Yohana 15:7
  • Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. - Yeremia 33:3
  • Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. - Yeremia 29:13
  • Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. - Isaya 65:24
  • Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. - Mathayo 18:19,20
  • Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. - I Yohana 5:14,15
  • ombeni bila kukoma; I Wathesalonike 5:17
  • Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu. - Zaburi 66:18,19
  • Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. - Luka 22:31,32
  • Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. - Waebrania 7:25
  • Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. I Timotheo 2:8
  • Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. - Warumi 8:26,27
  • Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. - Marko 11:24
  • na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. - I Yohana 3:22
  • Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. -Mathayo 26:39
  • Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. - Mathayo 6:6,7
  • Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. - Waebrania 4:16
  • kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; - Waefeso 6:18
  • Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. I Timotheo 2:8
  • Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu. - Zaburi 55:17
  • Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao. -
    Zaburi 102:17
  • Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. - Zaburi 116:1,2

Mungu atajibu maombi yetu / God Will Answer Our Prayers


  • Zaburi 55:17 ­- Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
  • Zaburi 102:17 - Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.
  • Zaburi 116:1, 2 -Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
  • Isaya 30:19B - Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.
  • Isaya 65:24 - Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
  • Yeremia 33:3 - Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
  • Mathayo 6:5 - Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
  • Mathayo 18:18, 19B, 20 -Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
  • Yohana 14:13, 14 - Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
  • Yohana 15:7 - Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
  • Yohana 16:23B, 24 - Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
  • Yakobo 4:8A - Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
  • 1Yohana 3:22 - Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
  • 1Yohana 5:14, 15 - Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

Kuomba Katika Imani / Pray In Faith


  • Isaya 45:11 - Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.
  • Yeremia 29:13 - Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
  • Mathayo 21:21B, 21D, 22 -Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
  • Marko 11:24 - Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
  • Luka 11:9, 10 - Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
  • Warumi 4:20, 21- Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
  • Waefeso 3:20 - Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
  • Waebrania 4:16 - Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
  • Waebrania 11:6 - Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
  • Yakobo 1:6, 7 - Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
  • 1Yohana 5:14 - Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.



Maombi ya siri / Private Prayer


  • Zaburi 5:3 - Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
  • Zaburi 63:1 - Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
  • Zaburi 119:2 - Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.
  • Mathayo 6:6 - Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Maombi ya Tamaa / Desperate Prayer


  • 2 Samweli 22:5-7 -Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;
  • Zaburi 22:24 - Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia.
  • Zaburi 50:15 -Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
  • Zaburi 62:8 -Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
  • Zaburi 106:44, 45 - Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao. Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;
  • Zaburi 119:10 - Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
  • Isaya 55:6 -Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
  • Isaya 64:7 - Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.
  • Yeremia 29:13 - Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
  • Maombolezo 2:19 - Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa makesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.
  • Maombolezo 3:40, 41 - Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia Bwana tena. Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni Mioyo yetu na mikono.
  • Yoeli 2:12 - Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
                        Mathayo 17:21 - Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.

No comments:

Post a Comment