NYAKATI NGUMU
- 1
Wafalme 17:16A - Lile
pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa
na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
- Ayubu
5:20 - Wakati wa njaa atakukomboa na
mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.
- Zaburi
9:9, 10 - Bwana atakuwa ngome kwake
aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida. Nao wakujuao jina lako
wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao.
- Zaburi
37:18, 19B - Bwana anazijua siku za
wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. Hawataaibika wakati wa ubaya,
Na siku za njaa watashiba.
- Zaburi
37:25 - Nalikuwa kijana nami sasa ni
mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba
chakula.
- Zaburi
46:1-3 - Mungu kwetu sisi ni kimbilio
na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa
ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake
yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
- Zaburi
62:8 - Enyi watu, mtumainini
sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
- Zaburi
91:2 - Nitasema, Bwana ndiye kimbilio
langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
- Zaburi
105:39-41 - Alitandaza wingu liwe funiko,
Na moto utoe nuru usiku. Walipotaka akaleta kware, Akawashibisha chakula
cha mbinguni. Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama
mto.
- Isaya
44:3 - Kwa maana nitamimina maji juu
yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho
yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;
- Mathayo
6:30, 31 -Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi
majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi
sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule
nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
- Warumi
8:35-39 - Ni nani atakayetutenga na
upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au
hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa
mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika
mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala
malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala
wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho
chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu
Bwana wetu.
- 2
Wakorintho 4:8, 9 -
Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;
twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;
- Ufunuo
wa Yohana 12:6 - Yule mwanamke akakimbilia
nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko
muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
- Ayubu
26:8-10 - Huyafunga maji ndani ya
mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. Husitiri uso wa
kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake. Amepiga duara
kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.
- Zaburi
46:1-3 - Mungu kwetu sisi ni kimbilio
na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa
ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake
yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
- Zaburi
89:9 - Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi
cha bahari. Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.
- Zaburi
93:4 - Kupita sauti ya maji mengi,
maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye
mwenye ukuu.
- Zaburi
107: 29 - Huituliza dhoruba, ikawa shwari,
Mawimbi yake yakanyamaza.
- Isaya
4:6 - Kisha kutakuwa na hema kuwa
uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na
kujificha wakati wa tufani na mvua.
- Isaya
25:4 - Maana umekuwa ngome ya
maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati
wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao,
Kama dhoruba ipigayo ukuta.
- Isaya
43:2 - Upitapo katika maji mengi
nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika
moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
- Nahumu
1:7 - Bwana ni mwema, ni ngome siku
ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.
- Mathayo
8:26, 27 - Akawaambia, Mbona mmekuwa
waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari;
kukawa shwari kuu. Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani
hata pepo na bahari zamtii?
- Luka
10:19 - Tazama, nimewapa amri ya
kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.
No comments:
Post a Comment