Luka
13:22 - Mtu mmoja akamuuliza Bwana Yesu
Je! Watu wanaookolewa ni wachache? Bwana akamjibu akamwambia jitahidini kuingia
katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawambia kuwa wengi watataka kuingia
wasiweze.
Mahali
pengine maandiko yanasema tangu enzi za Yohana mbatizaji habari njema
ya ufalme inahubiriwa, na wenye nguvu wauteka huo ufalme.
KUMTUMIKIA
MUNGU
Katika
Mathayo 19:27 tunaona maneno ambayo mtume Petro alimuuliza Bwana Yesu
kuwa walikuwa wameacha vitu vyote na kumfuata Yesu, Je! Watapata NINI? Mara
nyingi napenda kusema kuwa hakuna mtu yeyote duniani mwenye akili timamu
anayependa HASARA. Petro alitaka kujua atakachokipata, baada ya kuwa ameamua
kuacha vyote na kumfuata Yesu. Kama ingetokea Bwana Yesu amjibu kuwa fanya
kazi maana UNAJITOLEA, nadhani hapo ndipo ingekuwa mwisho wa Petro.
Lakini kwa kumjibu alimwambia atapata mara mia, katika ulimwengu huu na uzima
wa milele baadaye.
Habari
hii pia tunaiona katika Marko 10:28-31 huku tofauti ikiwa ni kuongezwa maneno
PAMOJA NA DHIKI katika Marko. Ndiyo maana katika Galatia 6:9 mtume Paulo
aliandika maneno fulani ili kuwaambia Wakristo waendelee kufanya kazi ya Mungu
bila kuchoka, maana malipo yapo baada ya kazi hii katika dunia hii. Maneno hayo
ni:
Tena
tusichoke katika kutenda mema, kwa maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia
roho.
1Kor
15:58; “Basi,ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda
kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua kwamba taabu yenu siyo bure katika
Bwana”. Yaani kazi ambayo
italipwa ni ile iliyofanywa katika Bwana,( sio kazi yoyote, katika Bwana. Ndiyo
maana anasema ni wale tu wafanyao MAPENZI YA BABA YANGU). Kumbe unaweza
ukafanya kazi ya Mungu, lakini yakawa siyo mapenzi ya Mungu.
Katika
Ebrania 6:10 tunaona kuwa Mungu si dhalimu hata aisahau kazi ya mtu. Hii
ina maana kuwa Mungu hawezi kudhulumu mtu yeyote. Ndio maana imeandikwa “kila
mtu atavuna kile alichokipanda”.
Faida
ya Kumtumikia Mungu.
Faida
utakazozipata kama ukiamua kumtumikia Mungu kwa dhati. Faida hizi ni zile
utakazopata ukiwapo hapa hapa duniani. Najua tutalipwa pia na mbinguni, lakini
leo naongelea faida za hapa hapa duniani.
-Mithali
11:31 – Mwenye haki atalipwa duniani, na mkosaji pia.
-Mithali
11:25 – Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa. Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Maana yake ni chochote unachofanya kwa watu, ujue na watu
pia watakufanyia. Ukifanya ubaya, ndivyo utafanyiwa; Ukifanya wema ndivyo
utafanyiwa.
-Mith
12:14 – Utavuna chochote utakachokipanda.
-Mith
20:7 – Chochote utakachokifanya, kizuri
au kibaya, utawaachia watoto wako. Wakati mwingine unaweza kudhani uko salama,
kumbe utawaachia watoto wako ama BARAKA, au LAANA. Ukiangalia kwa makini
katika 1Falme 4:24-25 kuna maandiko maneno yanayosema kuwa Sulemani
alistarehe pande zote. Swali ni kwa nini alistarehe? Hii ni
kwa sababu baba yake alikuwa amepigana vita vya kutosha, alikuwa amesukumia
mbali maadui kiasi cha kuwa mbali sana na Ufalme wake Sulemani.
-Mith
13:22 – Huwaachia WANA WA WANA–
Unaona
sasa imekwenda kwa WAJUKUU. Ndiyo maana tunasema Mungu wa IBRAHIM,
ISAKA, na YAKOBO. Leo hii watu wengi wanahangaika kwa sababu ya yale ambayo
baba, babu zao walifanya; Wao wanahangaika leo, au wanafurahia leo.
-Luka
7:2-5 -Kuna maneno yanayoonyesha jinsi Wazee
walivyomwambia Yesu kumtendea jambo jema mtu ambaye aliwajengea sinagogi. Hivyo
kwa kuwa alijenga SINAGOGI basi alistahili kutendewa jambo hilo. Kumbukumbu
ni muhimu sana. Leo hii kuna watu wameshapita lakini hakuna kumbukumbu lolote.
Walikuwa na mali, walikuwa na uwezo, lakini leo hakuna kumbukumbu lolote kuwa
walikuwepo duniani.
-Mith
10:27-Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu.
Mpendwa Neno linasema wazi wazi kuwa kama utakuwa ni mcha Mungu miaka yako
itaongezwa, mahali pengine inasema AKASHIBA SIKU.
Katika
Isaya 54:12-17 tunaona faida tupu kama ukimcha Mungu, sitaikopi hapa,
tafadhali tafuta muda uisome uone. Waweza soma pia faida tele katika Isaya
43:2 na uone kuwa hakuna hasara yoyote katika kumcha Mungu.
-Ayub
5:19-27. Ayubu alikuwa ni mzee wa siku
nyingi hivyo alijua faida tele za kumtumikia Mungu. Ndiyo maana aliandika namna
hiyo hapo, ebu soma uone!
Watu
waliomtumikia Mungu na kuona faida zake, ambao habari zao tunazipata katika
Biblia. Pata muda usome maandiko kuhusu mifano hii:
-Mdo
9:36-Dorkas.
-Isaya
38:1-Hezekiah.
-Esta
3:12-Mordekai.
-Mdo
10:1-Cornelio.
No comments:
Post a Comment