·
Msizidi
kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana
ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. - I Samweli 2:3
·
Kijapo
kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. -Mithali 11:2
·
Kiburi
huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. - Mithali 13:10
·
Bwana
ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane. - Mithali 15:25
·
Thawabu
ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. -
Mithali 22:4
Mithali 22:4
·
Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye
roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. - Mithali
29:23
·
Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na
aangalie asianguke. I Wakorintho 10:12
·
Na torati haikuja kwa imani, bali,
Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. - Wagalatia
3:12
·
Jidhilini mbele za Bwana, naye
atawakuza. - Yakobo 4:10
·
Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa,
naye ajidhiliye atakwezwa. - Luka 14:11
·
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha,
amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama
hayo hakuna sheria. - Wagalatia 5:22,23
·
Msitende neno lo lote kwa kushindana
wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa
bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu
aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo
pia ndani ya Kristo Yesu; - Wafilipi
2:3-5
·
Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo
kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu. - Mithali
16:5
·
Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho
yenye kutakabari hutangulia maanguko. Mithali
16:18
·
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa
mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. - Mithali 16:25
·
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu
hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu. - Mithali 18:12
·
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi;
kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. - Yakobo 4:6
·
Wenye upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia yake. - Zaburi
25:9
·
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee.
Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu
huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni
chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku
mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo
yenu. - 1 Petro 5:5-7
·
Mfalme wa Israeli akajibu, akasema,
Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye. -
I Wafalme 20:11b
No comments:
Post a Comment