Thursday, June 30, 2016

MAANA YA MAOMBI NA AINA ZA MAOMBI NA KAZI ZAKE

Pasipo MKONO wa BWANA, utarudi mtupu ! …

” …BWANA YESU asifiwe sana !
Nakusalimu kwa Jina la BWANA, Mungu wa Ibrahim, Isaka na Israel…. Yeye ambaye hulituma neno lake ili kuyatenda mapenzi yake, kwa ajili ya Utukufu wa Jina lake.

Somo hili tutajifunza maeneo ma-NNE ya maombi, (yaani maombi ya NDANI na NJE ya milki au Ufalme wa Mungu) Narudia, tunajifunza maeneo ma-4 katika kuomba na kuutafuta uso wa BWANA. Nami nafundisha kama nilivyofundishwa & kuongozwa na Roho Mtakatifu kwa Utukufu wa Jina la YESU KRISTO, aliye HAI milele yote.

Utangulizi;

(a)    NDANI: Wale wote waliompokea BWANA wamefanyika kuwa watoto wa Mungu, ndani ya Ufalme wa Mungu, nyumbani kwa BABA. Hapa ni maombi ya kuhama kituo, ili BWANA azidi kutuinua naye akitukuzwa kwa hilo. Ni maombi ya IMANI katika unyenyekevu kwa BABA yetu atupendaye sana. Hapa tunaomba vipawa & karama, hekima, kuona, utii, utumishi bora nk, pia tunaomba mume/mke, makazi nk.
(b)   NDANI: Maombi ya kujitakasa na kung’oa mapando ya giza hufanywa na wana-wa-Mungu ndani ya Ufalme wa Mungu (Deliverance). Vifungo vya giza, Unajisi na Mapando ya giza huwavamia wateule pale unaposhindwa kuliishi NENO na kuanguka katika majaribu, pamoja na changamoto za maisha. Hivyo basi mapooza hayo yatokanao na dhambi ambayo husababisha mwovu hutumia mlango huo kutushambulia;  yaani magonjwa, moyo mchafu, huzuni, kukata tamaa, kukwazika, mafarakano, uvuguvugu.
(c)    NJE: Hapa tunasimama kama “makuhani” kwa ajili ya watu/ jambo linalofanyika NJE ya Ufalme wa Mungu. Tunasimama mbele za BWANA katika HOJA yenye nguvu katika NENO, tukiwa na sadaka ya ‘Damu ya Yesu’, inayofungua mlango kwa BWANA kutenda mapenzi yake ndani mwa mtu/jambo katika jamii hilo linalotukabili. Ni maombi ya kugeuza mioyo na kuwaleta watu/jambo kwa YESU. Kuombea ndugu/jamaa waokoke, wawekwe huru na dhambi; pombe, ufisadi, usaherati nk (haya yote yapo NJE ya milki ya Mungu)
(d)   NJE: (Ufunuo 5:10 “…Nao wanamiliki juu ya nchi”) Hapa “kanisa” linasimama kuomba ki-MAMLAKA. Hapa tunatawala kwa NENO la BWANA juu ya uumbaji wote ili kile alichosema BWANA ndio kisimame dhidi ya falme za giza, mamkala za giza, majeshi ya pepo wabaya na kila namna ya uasi, wote lazima walitii NENO la BWANA. Haijalishi giza hilo lipo kwenye ardhi, anga, maji au hewa na vinamilikiwa na ufalme upi NJE ya Ufalme wa Mungu, vyote vinatiishwa kwa NENO. Hapa ndipo tunapigana kwa Mkono wa BWANA katika Roho Mtakatifu.(Karibia ‘70% ya waombaji’ wamebobea sana eneo hili, kuangamiza uchawi, uganga nk)

Hivyo kila uombapo, jipange vizuri ujue unaomba jambo la NDANI au NJE ya Ufalme wa Mungu. Usiwe unakurupuka na  unachanganya habari mwishowe hukumbuki ulichoomba na usikipokee. Na ndilo kusudi langu kwako ili uweze kujipanga na kuomba katika “Roho” kutakapopelekea wewe kupokea ulichoomba.
Ni ndani ya “Roho ya Eliyah” pekee, ndio utakapoweza kuomba kwa pamoja maeneo yote maNne na ukapokea kile ulichoomboa. Ndani ya Roho ya Eliyah ndipo unapotembea na madhabahu ya NENO, ya udhihirisho wa Mungu kwa kile unachoomba. Unaposema Roho ya Eliyah ndio Roho inayobeba Wivu wa BWANA ndani mwako, ndio Roho ya Kumcha BWANA. Na inatenda kazi katika Marko 9:12marejesho” na Mathayo 17:11matengenezo” na Malaki 4:5-6upatanisho”. Vyote nitavionyesha hapo mbeleni.
Fanya bidii kujifunza kuhusu Roho ya Eliyah ili usipotoshwe wala usidanganywe, ukadhani upo ndani kumbe upo nje ya njia.

Kabla hatujaanza somo, tujifunze kwanza, na tuone vile jinsi Eliyah alivyotenda katika maeneo hayo yote  maNne kama sisi tunavyoenda kujifunza kwa NENO la BWANA;

1 Falme 18:36-40  36’…Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahim, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.

37’ Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie,

38’Ndipo moto wa BWANA ukashuka….. 39’Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu…
40’Eliya akawaambia, Wakamateni manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliyah akawachukua mpaka kijito cha Kishoni , akawaua huko

Pokea kuona; jinsi ya kuomba maeneo maNNe na kupokea ndani ya Roho ya Eliyah;
» (a) Eliyah alipoomba kwa NENO la BWANA, Mungu alimjibu na BWANA akatukuzwa na Eliyah akaheshimika kuliko ilivyokuwa awali, wote walijua kuwa ni mtumishi wa BWANA (Eliyah alihama kituo)

Imeshibitishwa na (na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako,)

Nami nakufundisha katika eneo la KWANZA, kuomba maombi ya kuhama kituo na Mungu wako akitukuzwa.

» (b) Nguvu za Mungu ziliposhuka katika MOTO ulao, madhabahu nyingine zote za Baali zilivunjwa ndani ya Israeli (kanisa) na ndipo Madhabahu ya BWANA ilisimama.

Imeshibitishwa na (Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka…na kuni, na mawe na mavumbi, ukayaramba na maji )

Nami nakufundisha katika eneo la PILI, kuomba maombi ya kujitakasa na kung’oa mapando ya giza ndani ya kanisa/yako wewe ili usihi katika utakatifu kama BABA yako alivyo mtakatifu.

» (c) Kwa maombi ya Eliyah, uweza wa BWANA katika marejesho ulishuka, Mungu alitenda kuwageuza mioyo wao wote wamrudie Yeye. Na walipoona ukuu na uweza wa Mungu, wote walimtukuza Mungu.
Imeshibitishwa na (na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie, na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu)

Nami nakufundisha katika eneo la TATU, jinsi ya kusimama kama kuhani ili wengine warudi kwa BWANA na pia BWANA aingilie kati jambo katika jamii na lisimame sawasawa na NENO la BWANA.

» (d) Katika uweza mkuu wa kiUngu, ndipo Eliya alipokuwa na mamlaka juu ya ufalme wote wa giza na akawachinja wote katika eneo la NJE ambalo sisi kanisa tunamiliki kote kwa Jina la Yesu.

Imeshibitishwa na (Wakawakamata; (manabii wa Baali)na Eliyah akawachukua mpaka kijito cha Kishoni , akawaua huko)

Nami nakufundisha katika eneo la NNE, jinsi ya kutawala kwa MAMLAKA ya JINA LA YESU katika NENO la BWANA na kuwaangamiza miungu, na watenda kazi wote wa ufalme wa giza.
Sasa umepata changamoto ya kujifunza zaidi na kuimarika katika BWANA. Tuendelee…
Maombi yasiyo na udhihirisho ni sawa na upepo uvumao usiotikisa unyasi wala kuangusha mti. Mwombaji hapati ushuhuda wowote wala heshima yeyote wala Mungu wako hawezi kithibitika na kutambulikana.
Nakushirikisha somo hili litakalokupa mwongozo katima MAOMBI na jinsi vile ikupasavyo kuenenda. Wengi tumepata neema na nguvu ya kusimama katika kuomba, lakini sio wote wamepata majibu ya kile walichokiomba.;
* wengi wanaomba halafu siku kadhaa mbeleni hawakumbuki kile walichokiomba, si rahisi kupokea…
* wengine wanaomba bila kusudi; jana kile, leo hiki, kesho kile… ataombea kila upepo na uvumi ujao…
* wengine wamekemea wakati wangetakiwa kunyenyekea, hawapokei majibu …
* wengine wameshajibiwa na hawajui, wanazidi kuomba kwa kasi bila kusikiliza sauti ya BWANA….
* wengine wamefunga na kuomboleza wakati walitakiwa kukemea kwa mamlaka ya kiUngu, n.k
BWANA akupe kujifunza na kubadilika ili uinuliwe katika viwango vya JUU ambavyo kanisa limeinuliwa sasa, ili wote tuweze kuomba katika viwango vya Roho ya Eliyah… Ni kipindi cha kutembea na 4WD yaani mafuta TANKI NNE…
Angalizo # 01 Enenda mbele za BWANA katika KWELI ili ajidhihirishe kwako, na kamwe usimdhihaki…
● Mungu anatazama wivu wa BWANA ndani ya moyo wa mwombaji,
● Mungu anatazama kumaanisha ndani ya moyo kutakoleta udhihirisho (transformation),
● Mungu anatazama kituo unachotaka kwenda kwa Utukufu wa Jina lake.
DAMU YA YESU ndio inayotutakasa, inayotupa haki, inayotupa kibali kusimama mbele za BWANA. Ipo nguvu ndani ya Damu ya Yesu inayotenda kazi ndani mwa mioyo yetu; (tafakari na ufahamu yafuatayo)
° Kupokea ni katika UTAKATIFU   ° Kutenda ni katika IMANI  ° Udhihirisho ni katika KUTHUBUTU

Simama katika KWELI na utamuona Mungu wa KWELI. Hapa nawaonya nyie mlio vuguvugu, wokovu FEKI, mnaokumbatia dini huku mnataka kumuona BWANA, na nyie mliojaa hila za nabii wa Uongo, maana majira zenu zimemezwa pale Ufunuo 19:20 . Huwezi kumuona MUNGU katika udanganyifu.

Hapa nafundisha kanisa (wateule) sio dini wana dhehebu 1 Petro 2:9 ”bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake…”. Hao ndio KANISA walio kombolewa kwa Damu ya Yesu ambao wanaongozwa na Roho Mtakatifu ndani ya Adamu wa Pili .

Angalizo # 02 :
Fahamu MAJIRA sahihi unayotakiwa kusimama uombapo kwa ajili ya udhihirisho mkamilifu…


Kuna majira & nyakati ambazo huwezi kupata majibu ukiwa unaomba, na zipo majira & nyakati za kanisa ambazo unatakiwa kusimama na kuomba ndio upate udhihirisho. Ni kinyume ikiwa unapanda mbegu wakati wa kiangazi, kuvuna wakati wa masika. Ni kinyume kabisa. Tena ni kinyume kutaka chai wakati wa kulala, usiku wa manane. Ujue una matatizo.
Zaburi 136:8-9 8’ “Jua litawale mchana; … 9’Mwezi na nyota zitawale usiku…”

Hapa nataka uone kuna mtawala na majira ya kutawala; yaani mtawala “Jua & Mwezi” na “mchana & usiku” ndio majira na nyakati za kutawala, kila mmoja na nafasi yake.

Nitakufundisha (kwa kifupi) habari ya miaka 1,000 (majira) ya kanisa kutawala pamoja na BWANA, na kuhusu Adamu wa Pili (mtawala), kinyume na Adamu wa Kwanza. Hayo yote nitafundisha mwishoni mwa somo, ili walio wachanga kiroho wapokee kwa nafasi na uelevu. Hapa nimekudokeza tu. Amen.







Wengi hutafuta majibu kwenye MAOMBI, na hiyo sio sawa. Siri ipo kwenye kufahamu NENO, kuamini NENO na kuomba sawasawa na NENO la BWANA, hapo ndipo penye majibu. Hebu tafakari haya;

> Maombi ; (kwa tafsiri nyepesi)
MAOMBI ni njia ya mawasiliano kati ya kanisa na BWANA, kwa njia ya kutamka ( kwa kinywa au moyoni ) yakiwa katika mtiririko wa hoja kwa NENO lake, ili tupokee katika IMANI kile tuombacho kwake.
 Bidii katika kuomba husukuma udhihirisho… Luka 18:1 …imewapasa kumuomba Mungu siku zote, wala msikate tamaa  tena imeandiikwa 1 Wathesalonike 5:17 “…ombeni bila kukoma

Uwe na ufahamu na msimamo wa unachokitaka, ndipo uhakikishe unakipata Yakobo 5:17 …Eliyah akaomba kwa bidii…, …, kisha akaomba tena .
> Neno la Mungu ;
Ni lazima uwe na NENO la Mungu linalohusiana na kusudi la maombi yako. Ukitamka NENO la Mungu katika UJASIRI & HAKIKA basi ujue NENO ndie Yesu Kristo mwenyewe…weka imani yako kwake.

Yohana  15:5 …maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.Hakika, pasipo BWANA YESU huwezi kufanya jambo likasimama, Yohana 14:14 …Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifaya”. Anapozungumzia jina lake, anamaanisha NENO lake Ufunuo 19:13 “…naye ana jina, asilolijua mtu, ile yeye mwenyewe, naye anaitwa NENO wa Mungu.  Hivyo simamia NENO la Mungu ukiwa na HAKIKA juu ya neno lake (imani) kwa kile uombacho mbele za BWANA.

> Mapenzi ya Mungu ;
Kila utumiapo NENO la Mungu, lenyewe ni lazima litende mapenzi ya MUNGU, kwa faida ya kuujenga Ufalme wa Mungu. Isaya 55:11 “Ndivyo litakavyokuwa neno langu….litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. ”

Tusome 1 Yohana 5:14-15 “…ya kuwa tukiomba  kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia…, tuombacho.., twajua kuwa tunazo haja tulizomwomba”. Wengi wanaomba ki-binafsi kwa mapenzi yao, hawapokei. Si heshima mbele za BWANA kila kusimamia NENO lake kwa kulazimishia mambo yako, pasipo kumuuliza Roho Mtakatifu. Jenga tabia ya kumuuliza Roho Mtakatifu, je ni nini mapenzi ya MUNGU katika hiyo changamoto unayopitia. 1 Wathesalonike 4:18 “…hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu .
> Utukufu kwa BWANA ;
Isaya 41:8 “Mimi  ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine…(uwe makini juu ya hili)

Hakikisha BWANA YESU ndie anayepewa Utukufu, yaani “nia” iliyobeba kusudi la maombi yako ni kwamba; BWANA, Mungu wako atukuzwe. Wafilipi 2:5 “…iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesukwa maana Ufunuo 4:11 “…Umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu , kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa maana wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote , na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.Mbinguni anatukuzwa, viumbe vyote vinamtukuza, na wewe mtukuze yeye

Jizoeze sasa ili kujenga tabia ya kutafakari kile uombacho kabla ya kuomba. Usikurupuke, na ujiulize je  kitampa Mungu Utukufu ? Usipopata amani moyoni, acha kwanza, jipange upya…

SOMO LINAANZA HAPA:
Maeneo ma-NNE ya maombi, katika kuujenga Ufalme wa Mungu…;
Uwe huru kuanza eneo la KWANZA au la PILI au la TATU au la NNE, vyovyote vile. Hakikisha umesoma maeneo yote maNNE.

(1)    Maombi ya NDANI ya milki ya Mungu, ukisemezana na BABA yako;
Luka 15:31
Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote, na vyote nilivyo navyo ni vyako 
Hivi ndivyo BWANA anakuuliza, je wataka nikufanyie nini ?  Na hapa tunajifunza JINSI YA KUPATA UNACHOTAKA NDANI MWA UFALME WA MUNGU. ( rejea SILOAM – 10 Shebati 2009 ) Hivyo kabla hujataka ni lazima º ujue wapi utapata unachokitaka º na jinsi kinavyopatikana.
Sasa kila kitu tuombacho kipo kwa BWANA, na vyote vyatoka kwake. 1 Nyakati 29:11-12 “…maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako, … Utajiri na heshima hutoka kwako wewe…” mke/mume atoka kwa BWANA, nyumba au gari vyatoka kwa BWANA, utumishi bora, hekima na maarifa vyote vyatoka kwa BWANA, ndio maana ni lazima ujue jinsi ya kuenenda ili kupokea ahadi za BWANA….

Kumb 28:1-14 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza  kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA , Mungu Wako atakapo…” Hapa hajasema “njooni huku mBarikiwe, leteni vitambaa vyeupe, leteni funguo za gari, mtabarikiwa…” huo ni UONGO, ila amesema *kusikia , *kutunza , *kuyafanya . Lazima ujifunze formula hii ya K3 “Kusikia na Kushika na Kutenda” sawasawa na NENO la Mungu, ndipo kuna kutukuzwa na kubarikiwa        ( K1 + K2 + K3 = 3K ) ndio lango la kupokea kutoka kwa BWANA.
Jiulize wewe kama mwana wa Mungu, Warumi 8:15 …mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani Baba je unataka nini kutoka kwa BABA yako aliye mbinguni, maana neema ya wokovi umeshapata na sasa unataka kukua na kuhama kituo? Imeandikwa  Mathayo 7:7-8 “Ombeni nanyi mtapewa….kila aombaye hupokea”  Je unataka nini ?

» Kumb 8:3-4kuzaa & kuongezeka”  soma NENO, tafakari hadi liumbike ndani, amini na uombe,
» Kutoka 23:15utumishi bora”  soma NENO, tafakari hadi uone kitu ndani, omba kwa ujasiri,
» Zaburi 4:8kupata usingizi mzuri”  soma NENO, ndio alichosema BWANA, tamka na uamini,

Sasa unaposoma NENO la Mungu (K1) na unapochukua hatua kulitafakari na kuliamini moyoni (K2) ndipo unaposimama mbele za BWANA na kuomba sawasawa na NENO (K3) = Muujiza wako.

Unapoachilia NENO la Mungu katika maombi ujue ni lazima lifanyike mwili (wewe usihofu wala kuumiza akili zako kuwa itakuwaje, maana ni Mungu alitimizae NENO lake, si wewe) kupitia vitendea kazi ambavyo ni ;
¤ Jina la Yesu          ¤ Damu ya Yesu          ¤ Roho Mtakatifu           ¤ Malaika wa BWANA.

Hebu tafakari kwanza ni nini umejifunza hapo juu, kabla ya kuendelea. Basi fahamu kuwa, maombi tuombayo hapa ni ya kuhama kituo; Luka 15:31 “Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote, na vyote nilivyo navyo ni vyakondio maana imeandikwa 1 Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari,… …kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu” kwani Ufunuo 4:11 “…kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.  BWANA anasema, je nikufanyie nini ?  anasema Isaya 43:26 “Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako”

Angalizo # 03 : Matamanio ya dunia vs Kiu ya kuujenga ufalme wa Mungu
Soma ujionee; mataifa huomba kwa kutamani ‘mavumbi ’, bali kanisa huomba ‘yaliyo juu’;
Je ulishajiuliza kwa nini NENO limetuonya sana kuhusu KULA na KUNYWA katika maisha yetu?

Mathayo 6:31-33 “Msisumbuke, basi mkisema, tule nini? au tunywe nini? na hakuishia hapo, akaendelea kutusisitizia kuwa  Warumi 14:17 “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa,

̊ Mataifa: Warumi 8:5-6 “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, …
-       Matamanio ya moyo wake ni mambo ya mwilini kwa ajili ya mwili…akiomba “…” kusudi lake ni “…” mume/mke: aonekane na watu kuwa ameolewaana,mume handsome,anapendeza wakitembea nk gari/nyumba: atapata kwa hila, akijijengea fahari mbele za watu. Hofu ya kuibiwa inammaliza. akili/hekima: watu wamfahamu na wamtukuze kuwa yupo amesoma, aheshimike kwa watu nk Vyote aombavyo ni mavumbi, vyatoka ardhini : materials zote za kutengeneza gari ni mavumbi, 
simu ni mavumbi, sofa seats ni mavumbi, tv ni mavumbi, nyama-choma ni mavumbi, pombe ni
mavumbi, nguo ni mavumbi, music system ni mavumbi….na MWISHO wao wote watarudi
mavumbini maana asili yao wao ni Adamu wa Kwanza atoka kwa UDONGO na ni MAVUMBI, sawasawa na  1 Wakorintho 15:40-50 40’“Tena kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, … 47’ Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48’ Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walio wa udongo…” ukiomba kama/ katika kituo cha wanadamu au watu basi utavuna udongo.

Yakobo 4:2-3 “Mwatamani wala hamna kitu,
mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi. Hata mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”

̊ Wateule:
Wakolosai 3:2 “Yafikirini yaliyo juu, sio yaliyo katika nchi” kwa maana Yohana 17:16  “Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu”

-       Matamanio ya moyo wake ni kumtumikia BWANA na kulitukuza Jina lake, huku ukimpendeza BWANA. mume/mke:Utampata atokae kwa BWANA, ubavu wako, akupendae,akutunzae,anayemcha BWANA. gari/nyumba:Utavipokea vitumike kwa BWANA, vilivyowekwa wakfu & vyenye madhabahu ya BWANA akili/hekima: Utaomba ili kanisa lipate kujengwa kupitia vipawa na karama ulivyopewa. Vyote aombavyo vyatoka kwa BWANA, na vimejaa Warumi 14:17 Maana ufalme wa Mungu ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu mume/mke atoka kwa BWANA, na mnaishi kwa amani, nyumba / gari vyatoka kwa BWANA nawe unamiliki kwa haki, huku maisha yako yote unatembea katika matendo ya haki. Na kwa kuwa wewe si mtu wala mwanadamu, ila ni Mwana-wa-Mungu, hakika umetoka kwa BABA na utarudi kwa BABA Yohana 3:6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho”, na hapo SIO mavumbi.

Luka 18:7 “Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, …? 
Mpendwa wa YESU, ni muhimu sana ubadilishe fikra zako katika kuomba, maana hutopokea. Ni lazima, narudia ni lazima uuelekeze MOYO wako kwa BWANA na NIA yao iwe ile ya KRISTO, uweze kupokea. Vinginevyo utapata lakini ni FEKI na kwa masharti, ama ufisadi au uasherati au kupitia nabii wa uongo, mizimu  & nguvu za giza, utapata  VISIVYODUMU sawasawa na mataifa. Hapa nakufundisha Zaburi 119:105 uweze kutembea katika njia za BWANA kwa Utukufu wake.


Kanisa sasa lipo majira & nyakati za kupokea kile uombacho PAPO KWA HAPO , sawasawa na HAKIKA uliyonayo inayoachilia nguvu na ujasiri kudai HAKI yako mbele za BWANA. Hizi ni zama za utimilifu wa UNABII wa Kitabu cha Mungu. Waefeso 3:20 “…kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Tupitie kwa uchache na kwa mifano aina ya maombi tuombayo NDANI ya milki ya Mungu. Ni kusudi langu kukupitisha ili uone umuhimu wa kuomba kwa NIA ya kuujenga UFALME WA MUNGU zaidi ya kuomba ki-binafsi zaidi…yaani maombi ya u-mimi u-mimi… Kumbuka si dhambi kuomba mambo ya mwilini ukiwa ndani ya milki ya Mungu, ingawa hayo husababishwa na uchanga wa kiroho na kutokumjua Mungu vizuri…na masomo haya yanatujia ili tujifunze na tukue kiroho.

Luka 12:29-32 29’ 'Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi, 30' kwa maana,hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo. 31’ Bali utafuteni Ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. 32’ Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.

(‘majira na nyakati hizi’)“Udhihirisho wa Nguvu za Mungu  unaotenda kazi kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha” Quote (Mtume  Eliyah - 29 Tammuz 2011), Je ni sawa kuomba kila wakati  maombi ya u-mimi u-mimi…wakati kanisa linatakiwa kuzidi kujengwa na kuimarika kabla ya unyakuo ? Kwa maana nyingine, nakwambia “tumika shambani mwa BWANA na ukamzalie Mungu matunda” naye atakutimizia haja ya moyo wako, maana Yeye anaujua moyo wako na anashughulika sana kwa ajili yako.

Na huku ndiko kuomba kwa hekima, Mathayo 6:9-13 “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje; MAPENZI YAKO YATIMIZWE hapa duniani kama huko mbinguni…”

● Suleiman aliomba kwa jinsi ya tofauti sana…hakika aliomba kwa msaada wa Roho Mtakatifu, nasi kupitia hayo tumejifunza kuwa tutake mambo ya rohoni kwa ajili ya kumtukuza Mungu wetu

2 Nyakati 1:10-12 10’Basi sasa nipatie hekima na maarifakwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?...



Suleiman alijua nafsini mwake kuwa Ufalme aliopewa ni kwa ajili ya kumtumikia BWANA, na watu anaotawala ni wa milki ya MUNGU, ndio maana aliomba HEKIMA na MAARIFA.
Hivyo kwa uweza wa Roho Mtakatifu aliwezeshwa kujua kuwa Ufalme wa Mungu ni Haki, Amani na Furaha katika Roho Mtakatifu

Warumi 14:17
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu



11’Mungu akamwambia Suleimani, …wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha ya wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu niliokutawaza juu yao

12’basi hekima na maarifa umepewa, nami nitakupa mali na utajiri, na utukufu, …”

Ooooh! our GOD is so awesome. Kwa maana SULEIMAN aliomba “…” alipewa “…” sawasawa na alivyoomba. Mungu aliposema “nami nitakupa” aliongea kwa nafsi yake, yaani He/ GOD spoke his heart, Mungu alipendezwa moyoni na maombi aliyoomba Suleimani, na kwa kuwa aliomba akitambua kuwa anasimama kwa ajili ya Ufalme wa Mungu na kwa ajili ya Utukufu wa Mungu, akazidishiwa sawasawa na Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na HAKI yake; na hayo yote mtazidishiwa” Namtukuza sana Mungu kwa kutupa ufahamu huu. Je umejifunza kitu?

● Watu wa mataifa daima huomba mali kwa ajili ya kufanya anasa. Ndio kula na kunywa, (pombe, nyama choma, ufisadi, hila & uasherati). Nao hulazimika kwenda kwa waganga na kuabudu sanamu ili wapewe utajiri FEKI, leo anaitwa tajiri akistarehe, kesho, kesho ni mgonjwa; moyo, kisukari, presha, kansa…huyoooo ndio tiketi ya kuzimu (Luka 16:19-28 “…Palikuwa na mtu mmoja tajiri, … … yule tajiri naye akafa akazikwa…kule kuzimu…katika mateso makali…” kajisomee) Tusiwaze kama wao tukavuna umauti.

● Unapoomba, kwanza weka kipaumbele kwa BWANA…omba mafuta zaidi umtumikie Mungu wako na Yeye akizidi kutukuzwa, imeandikwa 1 Wakorintho 12:31 “Takeni sana karama zilizo kuu” Omba kwa kumaanisha upokee hizi karama ili utumike nyumbani mwa BWANA. Tena omba uimarike katika NENO na IMANI Waefeso 6:10 “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake,

Omba uweza wa Kusikia, Kushika na Kulitenda NENO la BWANA ili ufanye kazi ya BWANA wako.

Endelea kumuomba MUNGU akuwezeshe uwe tunu kwake na kuupendeza moyo wake kama ;

Daudi (1 Samweli 17:45-51 “…bali mimi ninakujia wewe ‘Goliath’ kwa jina la BWANA wa majeshi…” Mungu alijibu papo hapo na Goliath aliuawa. Jambo lile lilimpendeza Mungu na yote yalitendeka kwa UTUKUFU wa Jina la BWANA)
Eliyah (1 Wafalme 18:36-40 “…Unisikie, Ee BWANA unisikie, … ndipo moto wa BWANA ukashuka…” Mungu alijibu papo hapo na manabii wa Baali wakauawa. Jambo lile lilimpendeza Mungu na yote yalitendeka kwa UTUKUFU wa Jina la BWANA)
Mungu wangu akujalie kuomba sawasawa na NENO lake kwa UTUKUFU wa JINA lako LAKE. Ubinafsi ndio ulimmaliza shetani ‘Lucifa’ (Isaya 14:11-15 “Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, … ulisema moyoni mwako, … nitafanana na yeye Aliye juu, Lakini utashushwa mpaka kuzimu;…” ) bali wewe ufanye bidii katika unyenyekevu mbele za BWANA huku ukiyatenda mapenzi yake, huko ndio kumpenda Mungu.

“Ndivyo litakavyokuwa neno langu….litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. ”
asema BWANA (Isaya 55:11) sasa jihadhari kulitumia NENO la Mungu kwa ubinafsi wa moyo mdanganyifu, ila uhakikishe unalitumia ili Yeye atukuzwe na Yeye akubariki.

Weka vipaumbele katika maombi yako, kwa maana BWANA anachunguza mioyo…Mathayo 6:31-33 “Msisumbuke, basi mkisema, tule nini? au tunywe nini? … kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta. ; kwa sababu BABA yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na HAKI yake; na hayo yote mtazidishiwa”

Amen, amen, amen.

Hitimisho: Tafakari nini unataka BWANA akufanyie ? Je ni mume, mke, utumishi bora, au unataka hekima & ufahamu, je unataka uinuliwe katika vipawa, au promotion kazini?

Tafuta UFAHAMU kwanza, je NENO la Mungu linasemaje, na uliamini NENO ndipo uombe ukiwa na IMANI katika NENO itakayokuwezesha kupokea. Weka msisitizo katika kuomba, udumu katika kuomba hadi upokee…usiombe ombe kila kitu, kila siku na hukumbuki uliomba nini jana. Badilika

Somo SEHEMU YA PILI linaendelea ukurasa unaofuata…


 
(2)          Maombi ya NDANI ya milki ya Mungu, uking’oa mapando ya giza ndani mwako;
Kanisa (wewe & mimi) tunatakiwa kuenenda katika utakatifu, utakaotuweka mbali na kunyanzi & mawaa. Waefeso 5:25b “…Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno, apate kujiletea kanisa tukufu lisilo na ila, wala kunyanzi…bali liwe takatifu lisilo na mawaa

Kukosa utakatifu, ndio mlango unaosababisha kanisa (wewe & mimi) kushambuliwa na mapando ya giza. Hapo ndipo unasikia watakatifu wanakemea “Toooka, PEPO toooka, kwa Jina la Yesu” . Unakemea mapepo yatoke maana yameingiza umauti kwa mwana wa Mungu aliye ndani ya milki ya Mungu.
 
Mika 4:1-2 “Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi…”(utawekwa & utainuliwa ni Unabii uliotimia sasa, kanisa limewekwa & limeinuliwa sasa)
Hiki ni kipindi ambacho ni lazima uishi katika UTAKATIFU sawasawa na 1 Petro 1:15 “…kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote” ili udumu kuishi JUU ya vilele vya milima na vilima(yaani JUU ya Uchawi, Uganga, Magonjwa, Mauti, Kuzimu, Mapepo, Falme & Mamlaka za giza nk), kinyume chake utapigwa na maadui.
Yakobo 2:10-11 “Maana mtu (mwana wa Mungu) awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote, …aliyesema usizini, pia alisema usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria” (sheria=neno la Mungu)

Unaposhindwa kuliishi NENO ndipo unaposhindwa kudumu kuinuliwa juu lilipo kanisa sasa. Mpendwa, usijihesabie haki maana Yakobo 1:22 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikilizaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu” Unaposhindwa kuwa JUU pamoja na kanisa, fahamu wazi huku chini ndipo kuna wezi & wanyang’anyi wenye kazi ya kuua, kuchinga, kuharibu na kuangamiza…

Tupitie mifano michache inayosababisha tukose kuliishi NENO, inayosababisha tukose UTAKATIFU, unaopelekea milango ya kushambuliwa na giza kuwa wazi;

1 Yohana 5:18 “Twajua ya kuwa, kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi” ukishindwa kujilinda ujue mwovu amekugusa, imeandikwa;
Warumi 3:23 “kwa sababu wote tumetenda dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” na ule utukufu wa Mungu unapungua kwako, ndipo magonjwa, dua mbaya, laana, chuma-ulete, kuibiwa nafsi nk na mabaya yote hutupata.
Haya yafuatayo husababisha mwovu kutushambulia, nasi inabidi kuomba kwa bidii kun’goa uovu huo…

Makwazo: Luka 17:1 “...Makwazo hayana budi kuja… Daima kuzimu wanatafuta mlango wakushambulie, hivyo Ufalme wa Giza hupanga kwa makusudi kukuletea jambo litakalo-kukwaza, ambalo litasababisha upatwe na hasira, chuki au uadui, nk Sasa ni lazima ujipange uwe na Warumi 5:3-5 saburi & uthabiti wa moyo ili jambo likikujia ufahamu kabisa kuwa “makwazo” amefika, anabisha mlangoni, ili kuingiza mapepo ndani mwako (hasira, ghadhabu,uchungu,makelele, matukano nk ).

Kusononeka moyoni: Mathayo 10:22 “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia hata mwisho…Pale ofisini wanakuchukia, sasa wewe unashangaa nini kuchukiwa ? Wao hawawezi kitu, wamejaa udanganyifu na hila (uzuri wao ni feki, ufanisi wao ni feki majungu tu,urafiki kati yao ni feki, unafiki tu, vicheko vyao ni feki, mioyoni wanawaka moto) hivyo wana wivu juu yako, wakikuona wewe unaenenda katika kweli na matendo mema, umejaa amani, una ujasiri nk.


Hivyo watakusema mabaya Zaburi 56:2-6 “Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, … Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya”  kwani umeitwa kwa Jina la Bwana (Kumb 28:10 ) Usipolijua hilo, ukahuzunika moyoni BURE, utajishusha chini BURE, mabaya yatakupata BURE. Soma Mathayo 5:11-12 usikamatiwe chini tena.

Kusengenya: Ni aibu kuona baadhi ya walio-okoka  ni vidomo-domo sio mchezo, halafu hawajijui ila wanajihesabia haki. Je nawe unawasema vibaya watumishi wapakwa mafuta wa BWANA; Hesabu 12:1-8 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa…, BWANA akasikia maneno yao, …BWANA akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Mariamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, … Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? …Hasira ya BWANA ikawaka juu yao, …Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriam, na tazama, yu mwenye ukoma” 

Sijui kama umeona kuwa BWANA aliwaita na aliwatoa nje la Hema (umeelewa) ndipo Miriam alipigwa na ukoma nje ya lango.Udumu kuihi katika UTAKATIFU sawasawa na NENO Mungu, maana anajua maneno yooote yaongelewayo katika siri Mathayo 10:26 “…kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikanaMungu anafuatilia hata meseji za simu yako, je unaishi maisha matakatifu ?

Ibada ya sanamu: Wengi hudhani ibada ya sanamu ni uchawi tu, au waabudu mwezi na waabudu mizimu, tu lakini neno linasemaje Wakolosai 3:5-8 “Basi vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, kutamani, ndiyo ibada ya sanamu, kwa ajili ya hayo huja ghadhabu ya Mungu. Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo, Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu hivyo ili uwe JUU ni lazima kumaanisha katika kushika NENO na kulitenda.

Kutazama ya dunia: Malaki 3:13-16 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA…, Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi  ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao…, Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia….Si sawa kinywani unatamka haya, moyoni unasononeka na kutazama yanayokuzunguka, hapa ndipo pia tunatakiwa kujitahidi tushinde.

Kuishi kwa ‘kawaida’: Hapa namaanisha kutokuwa na KWELI ya kumuishi Kristo, badala yake unaishi ki-shua shua pasipo kuwa shirika na BWANA. Imeandikwa Zaburi 135:1 “Halleluyah, Lisifuni jina la BWANA, Enyi watumishi wa BWANA sifuni” tena imeandikwa Zaburi 150:6 “Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA” Sasa kwa NENO hili hebu tafakari ni mara ngapi unafungua kinywa chako ukimsifu BWANA,kwa wengine kwa jinsi ile BWANA anakutendea katika maisha yako, au unaishi ki-kawaida kama raia wa dunia ? Hebu tafakari kuwa wewe mMoja tu humaanishi kwa hilo lakini malaika MILLIONI MIA na MOJA wanamsifu BWANA na kumtukuza Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi...hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu Ni vema kumuhimidi na kumsifu BWANA, Mungu wako angali wewe unaishi na katika maisha yako na matendo yako. Tembea katika njia za BWANA ili muwe pamoja Amosi 3:3

Mengineyo:
ء Mathayo 7:1-2 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi jilinde kinywa chako, jitenge na ubinafsi, kujiona bora kuliko wengine, ukijiona upo sawa wewe tu Wafilipi 2:3 “...kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake”
ء Walawi 17:12 “Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aliye katikati yenu asile damu” Nakuonya, kamwe Usinywe KISUSIO, pia usishiriki kuwapa kuku chakula chenye damu… Soma Walawi 17:11-14 ujihadhari kuruhusu “Waabudu Mwezi” kukuchinjia kuku ama mbuzi, maana ”makufuru wanayotamka” wakati wa kumchinja uje wamefanya agano la kuzimu na majini juu yako.
ء Kushirikiana na kuzimu & mizimu Mhubiri 9:5 “…; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwatena imeandikwa Isaya 25:14 “Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka ni kukosa ufahamu kushiriki kugawana nguo za marehemu (tena hajaokoka) ambaye sasa ni mzimu, tena kumfanyia ibada (misa) au ukumbusho wowote. Huo ni ushirika na kuzimu kupitia mizimu.
Kwa uchache tumeona mambo yanatusababisha kutoka nje ya hema na kushambuliwa na maadui

Kwa sababu ya hayo inatupelekea kufanya TOBA ya kumaanisha na kutafuta rehema za BWANA, inayoturejeshea mamlaka JUU ya mapepo  Luka 10:19-20 “…kwa vile pepo wanavyowatii…. Na hapo ndipo tunapofanya maombi tukiwa NDANI ya milki ya Mungu, lakini tuking’oa kila mapando za giza ndani mwetu na kila namna ya unajisi uliopo ndani mwetu. Kumbuka adui yupo ndani mwako, lazima ufanye “furmigation” ili usafishe nyumba na iwe SAFI.

Maombi haya ni ya MAMLAKA (govern/rule/administer). Ufahamu wa haki yako na ukiri wa NENO kwa kutamka, kunakupa nguvu ya kimamlaka juu ya giza liwalo lote, ndio maombi ya Yeremia 1:10

Tupitie kwa uchache, jinsi tunavyosimama katika mamlaka hii;  Lazima utembee na nguzo 4 za kanisa NENO (lazima uwe na NENO la kusimamia), IMANI (ndio HAKIKA juu NENO la Mungu), UTII (ndio Kusikia, Kushika na Kutenda unachoongozwa na Roho Mtakatifu) , UTAKATIFU (ndio uwepo wa Mungu kudhihirika kwako),

Ndipo tunapotamka kwa ujasiri katika maombi;

√ Imeandikwa Zaburi 118:17 “Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya BWANA na tena imeandikwa Hosea 13:14 “Nitawaokoa na nguvu ya kaburi; nitawaokoa na mauti…kwa Mamlaka ya Jina la Yesu, tunakemea na kuangamiza kila roho ya ganzi na umauti ndani ya “…” katika Jina la Yesu, tunaangamiza maagano yote ya Jini makata kwa Damu ya Yesu.

√ Ninasimama sawasawa na Mathayo 15:13 “…kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewaninang’oa kwa Mkono wa BWANA kila roho za hofu na mashaka, nabomoa hazina ya mawazo mabaya, ninaharibu kila mapando ya ubaridi & uvuguvugu katika kazi ya BWANA  nk

√ Tumepewa amri, mamlaka na uweza juu ya mapepo yote na magonjwa yote sawasawa na Mathayo 10:1 “…akawapa amri juu ya pepo wachafu…na Luka 9:1 “...awapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhina Marko 6:7 “…akawapa amri juu ya pepo wachafuNinaamrisha “Toka, kwa Jina la Yesu, Toka, pepo toka, ukimwi toka…kwa Jina la Yesu…Huna mamlaka, huna uweza, huna nguvu juu ya “…” Tooka, Tooka…

√ Imeandikwa Hesabu 23:23 “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli  Ninaharibu kazi zote za uganga na uchawi uliofanywa juu ya nafsi yangu, ninaharibu mazindiko na makafara yote kwa Damu ya Yesu, tena imeandikwa Isaya 44:25 “…na kuwatia waganga wazimu,…kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga sawasawa na dua na visomo walivyonisomea, ninawageuzia wao, nao wawe vichaa & wazimu, na kila ufundi & maarifa ya kuzimu yafanyike kuwa upuuzi, kwa Jina la Yesu… ( NENO + IMANI = Udhihirisho )

√ Kwa NENO la BWANA ninafichua na kun’goa kila namna ya siri na mafundisho ya upotovu ndani ya kanisa na nafsi za watakatifu, sawasawa na Ufunuo 2:2 “…umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo, Ufunuo 2:9 “…hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani, Ufunuo 2:14 “…unao huko watu washikao mafundisho ya Baalamu, …wayashikao mafundisho ya Wanikolai, hapa unajikung’uta mavumbi na roho chafu zilizokuvamia kupitia ushirika wako na BarYesu & Elima (Matendo 13:6-8)

Hivi ndivyo tunaposimama na kuomba kwa MAMLAKA YA KIUNGU. Tunaomba tukiwa ndani ya milki ya Mungu, lakini hatuombi kupokea, ila kung’oa giza, ukiwa na unajisi ndani mwetu au kutoka kwa yule tunayemuombea.

Ningeweza kusema kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa, haya maombi ni KUTAMKA KIMAMLAKA KWA NENO LA BWANA ili ATUKUZWE, na sio kuomba kama kuomba kwa uhitaji. Tafakari, umejifunza nini katika eneo hili?

Amen, amen, amen.

Somo SEHEMU YA TATU linaendelea ukurasa unaofuata…
(3)          Maombi ya ki-KUHANI juu ya walio NJE ya milki ya Mungu,

Mathayo 9:13 “…
Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”
Kusudi kubwa na maombi haya ni kuwarejesha wateule ambao bado wamekamatiwa na dunia katika giza. Umuonaye leo kuwa ni mlevi, mchawi au kahaba wa mjini, ufahamu kuwa wengi wao ni wa thamani mbele za BWANA ila adui amewawahi na kupotosha njia zao ili wasimzalie BWANA matunda. Unahitaji kusimama na moyo wa UPENDO wa BWANA YESU kuweza kusimama kuombea wengine. Yuda 1:22-23 “Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto, na wengine wahurumieni kwa hofu…” wengi tunajivunia kuwa tumeokoka, lakini si wengi wanakumbuka kuwaombea kwa mzigo ili BWANA aifungue mioyo ya wengine nao wapate neema ya wokovu.

Ezekieli 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka…” na Yeremia 5:1 “...kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye kwa uaminifu; nami nitausamehe”
Kuhani unatakiwa kusimama katika utakatifu sana na mwenye haki mbele za Mungu, uweze kutubu & kuomba rehema mbele za BWANA kwa uaminifu sana juu ya wale unaowaombea. Kama vile Kristo alivyobeba dhambi zetu msalabani, ndivyo unavyotakiwa kuwabeba hao wote katika TOBA ya kweli, ili BWANA awarehemu. Ukipita mjini na kumuona m-mama amechakaa na kutaabika, ama professor amechanganyikiwa au bubu au mtu amelazwa hospitali za vichaa, umuonapo mlevi chakari au changudoa au m-dada amevaa kichovu sana…wengi wetu tunawakwepa na kuwadharau au hatupendi kuhusiana nao, hizo ni roho za chuki na ubinafsi , ndio nafsi ya shetani ndani ya Adamu wa Kwanza. Tusome jinsi YESU alivyowaponya watu wa jinsi ambayo sisi tungewadharau;

» Wale unaowaona ni maskini, walevi, wachawi & makahaba, wengi (sio wote) wao ni wateule walio kifungoni Luka 13:11-16 “…palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyoosha kabisa…(hebu mtafakati mama huyu) …na huyu mwanamke, aliye uzao wa Ibrahim, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki…” tafakari kuwa miaka 18 yupo kifungoni, akiteseka sana … tena ni mteule wa BWANA (uzao wa Ibrahim), amepindana hajiwezi. Sifahamu ni kwa kiasi gani unawaonea hao huruma na kuwaombea, au unadumu kujiombea binafsi ?
» Isaya 42:7 “kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa  hapa usijihesabie haki, maana huenda nawe upo kifungoni…dini, mila, tabia za asili, kiburi cha maisha nk (chuki, kutosamehe, masengenyo, kiburi cha fedha au elimu, hasira nk ) wengi wamekamatiwa hapa Mathayo 15:9 “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho, Yaliyo maagizo ya wanadamu” hapo ndipo kwenye Krismasi, kubatiza watoto wachanga. Mume aliyekamatiwa na pombe au nyumba-ndogo ujue naye yupo kifungoni kama sio kuzimu kabisa. Yatupasa sisi kanisa kuwaombea hao ili BWANA awafungue nafsi & roho zao zilizopo kwenye magereza.
» Kasome Luka 8:27-36 “…alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini…, Pepo wakamtoka mtu yule…wakamwona mtu yule aliyetokwa na pepo…amevaa nguo, ana akili zake…” umuonapo mtu anayefanana na huyu, usimchukie ila muhurumie na jitahidi kumuweka kwenye maombi.
Mungu akujalie kutenda sawasawa na Wafilipi 2:4 “Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine  (sio katika umbea na kusengenya, ila katika kuwapenda, kuwahurumia na kuwaombea, huo ndio moyo wenye wivu wa BWANA ) Luka 15:10 “…Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye” Tafakari ni kwa jinsi gani hu-husiki kabisa kusababisha furaha mbinguni, kwani maombi yako yote ni ya u-mimi mimi, kupeleka kila namna ya binafsi yako kwa BWANA. Kinyume chake tafakari jinsi unavyohusika sana kuomba kama kuhani ili watu walio NJE ya Ufalme wa Mungu watubu na kupokea neema ya wokovu.

Kipimo: Je una furaha kiasi gani unapoona watu wengi wanakwenda mbele kuokoka ? furaha  ama kawaida ndani mwako ndio tathmini au ‘dimension’ ya kuhusika kwako kuwapeleka watu kwa YESU sawasawa na wivu wa BWANA ndani mwako katika kuombea wengine waokoke.
̊ Vifo vya watoto wachanga, mimba kuharibika ni kwa kuwa wahusika hawana MTETEZI, na wewe hujawaombea.
 
̊ Vibaka, wavuta bangi, machangudoa…wapo vifungoni, hawana tumaini, hawana wa kuwaombea….

̊ Manesi wasiojali waja-wazito, wahudumu wenye ukatili, hao wote wamefungwa na na giza na roho za kupenda fedha

̊ Bosi wako mwenye chuki na manyanyaso kwako, ametawaliwa na mizimu na kuzimu, anahitaji kutolewa gizani

̊ Viongozi wa nchi wabinafsi, mafisadi , wasio na moyo wa kutumikia wananchi, nao hao nafsi zao zipo kuzimu.
̊ Wanafunzi hawaelewi masomo, unahamisha shule hadi shule, hiyo yote haisaidii…kwa maana akili zao zimeibiwa
  zinafundishia mtaa wa pili kwenye darasa la tuition, na huko wote wanaelewa kwa akili za watoto wako.

̊ Unaposikia leo kijana amejinyonga kwa wivu wa mapenzi, kesho msichana wa kazi amekunywa sumu, kesho kutwa mhasibu anajitupa ghorofani….fahamu kuwa hao wote walikamatiwa na vifungo vya mauti. Walihitaji maombi yako

Hayo yote ni kwa sababu kanisa “wewe au mimi” hatujizoezi katika kumsikilizi Roho Mtakatifu atuongozaye katika kuomba. Tunataka kuomba tutakayo sisi, tena keshi yake ni wepesi kusikia habari mbaya kwenye radio au tv nasi tukajitia kuhuzunika sana. Lakini je mbona tunakosa upendo wa kuombea wengine, mbona ni wepesi kwenda kanisani ibada zoote, na mikesha yoote pasipo kuwaombea na kuwaleta wengine kwa BWANA ?
Basi kumbuka sasa kuwa;
º Mungu anatazama wivu wa BWANA ndani ya moyo wa mwombaji.


Amina na amina na amina.

Somo SEHEMU YA NNE linaendelea ukurasa unaofuata…

 


(4)          Maombi ya vita dhidi ya ngome za giza NJE ya milki ya Mungu ;
Kumb 20:1“Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe…”
Watakatifu wengi wamedumu sana eneo hili, wakirusha kila silaha na makombora pande zote wajuazo ili kushambulia ufalme wa giza. Hiyo ni sahihi kabisa, ila nikutahadharishe mapema kuwa, uwe mwangalifu sana…usijichokozee VITA pasipo kusudi la BWANA.

Jifunze jambo hili  1 Samweli 23:2 “Basi Daudi akamwuliza BWANA, kusema, Je! Niende nikawapige hap Wafilisti? Naye BWANA akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila” rudia kusoma uyaone haya; Daudi alijua kuwa Pasipo Mkono wa BWANA hawezi kuthubutu kupigana, na pia hakupigana kwa mapenzi yake tu, ila kwa kusudi la BWANA kuuokoa Keila.

2 Samweli 8:14 “…naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.” Nakukumbusha kuwa BWANA anapigana vita ili YEYE atukuzwe, sio wewe, kumbuka hilo likusaidie 2 Nyakati 20:29 “Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa BWANA amepigana juu ya adui za Israeli”
Ndio maana akasema Isaya 42:8 8’“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu” nimekuonyesha hili kwanza, ili ufahamu kuwa daima MUNGU hulituma NENO lake litende kwa UTUKUFU wake, na hakuna Mungu zaidi yake wa kutukuzwa ama kusifiwa ila Yeye, maana ni BWANA. Kumbuka hilo; vita si vya kwako ila ni vya BWANA.

Tusome kisa hiki cha Samsoni na Wafilisti, na utaona kuwa BWANA alijibu maombi ya Samsoni papo kwa hapo alipoomba kujilipizia kisasi juu yao kwa ajili ya macho yake. Tukumbuke kuwa BWANA, Mungu wa Israel, Mungu wa Kanisa ndiye pekee wa KUTUKUZWA, na wale wafilisti walikutana ili kumtukuza mungu wao “Dagoni”, ndipo BWANA akajibu maombi ya Samsoni ili kujitwalia UTUKUFU na kuiaibisha miungu ya sanamu, kwani BWANA hawezi kuaibika kamwe.



Waamuzi 16:23-24 “Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu…wakamuhimidi Mungu wao…”

Wafilisti walimkamata Samsoni kama adui yao, lakini yeye alisimama kama “Mnadhiri wa BWANA”, alibeba jina la BWANA…
Hivyo VITA vilikuwa ni vya BWANA na si vya Samsoni. ( Daima vita si vyako wewe )

Waamuzi 13:7 “
…maana mtoto huyo ‘SAMSONI’ atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.”

Kwa sababu hivyo basi, pale hakusimama Samsoni kama Samsoni, ila BWANA ndie aliyekuwa adui wa Wafilisti na ndie ambaye walikuwa wanamdhihaki…

Yohana 7:7 “Ulimwengu
hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, …”


Fahamu sasa jinsi ya utendaji wa MUNGU katika maombi yako, ni kwa UTUKUFU wake;
Waamuzi 16:27-30 27’Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu… 27’ Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili… 30’ Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti., …”

Hakika MUNGU alitenda papo kwa hapo, sawasawa na maombi (nakuomba,”) yote ya Samsoni aliyoomba mbele za BWANA, na hata alipojitamkia mwisho (Na nife,”) na ikawa kama alivyotamka kwa maneno ya kinywa chake Mithali 18:21 “mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi”, Jamani NENO ni upanga, linakula kote kote, kwa Wafilisti na kwako pia, kaa sawa.

Sasa jifunze kuwa maombi yako ya VITA, kwanza vita si vyako ila ni vya BWANA, hivyo basi ni lazima uweke NIA ya kumpa BWANA, Mungu wa Eliyah Sifa zote, Heshima na Utukufu kwa maana anastahili.

Nakutahadharisha kuwa, masaa 12 ya mchana na masaa 12 ya usiku, ufalme wa giza hukaa vikao na kupanga mikakati thabiti juu ya kanisa (wewe na mimi) Isaya 8:10 “Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika;…”  na imeandikwa Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuzipinga hila za shetani”  ( hila za shetani = the devil’s schemes, sasa tafakari kiundani maana ya hila au schemes ) Maadui wakijua muda wowote watashambiliwa katika ngome zao, hudumu kuwapotosha watakatifu ili wasisimame kwenye kusudi la Mungu. Nikupitishe kwenye mifano ya hila, hila;

» Unasikilizishwa maafa ya ‘mabomu ya Mbagala’, nawe badala ya kusikiliza mwongozo wa Roho Mtakatifu, unakurupuka kuombea kila kitu, wakati ulitakiwa kuombea mabomu yasitokee tena ‘Gongo la Mboto’. Unasahaulishwa kuomba ya mbeleni, unaonyeshwa matukio yaliyokwisha pita.
» Wengi huombea Uchaguzi Mkuu wa Nchi, huku wametawaliwa na HOFU, hivyo wote hudumu kuombea AMANI ya nchi, na wanasahau kuombea USAHIHI wa mchakato wa kuandikishwa wapiga kura, kuombea HAKI katika kuhesabu kura, kuombea KWELI ya matokeo ya Uchaguzi, Kuombea Hofu ya Mungu itawale ndani ya Tume ya Uchaguzi. Kitambo baadae waombaji hao hao unawasikia wanalalamikia kila kitu kuhusu uchaguzi. Je umeona hila? Ni hila tupu hizi ! Hata kiti cha rais unatakiwa uombe iki akae HAKI & KWELI kwa NENO la BWANA, na sio ‘Uharibifu & Udanganyifu’.
» Leo utasikilizishwa kisa cha Mama Mjamzito, kesho Mtoto amegongwa barabarani, kesho kutwa House-girl amejinyonga, kesho yake Mke amefumaniwa nk Unaombea kila upepo, kila vumbi…
Kumb 12:8 “Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama aonavyo vema machoni pake”  badala yake tunahitaji kuongozwa na Roho Mtakatifu Waefeso 6:18 “…mkisali kila wakati katika Roho,
Vita vya rohoni tunapambana na ngome, falme, mamlaka, wakuu wa giza, jeshi la mapepo, wakuu wa anga, malkia wa bahari na kila namna ya kuzimu na ushetani.
List ya walioangushwa na BWANA kwa aibu kuu;
(Hawa wote sasa si kitu, wamepigwa, wameanguka wote, hopeless, wananuka funza wote, BWANA amewaangamiza wao na ufalme wao, wamemezwa kwenye ziwa la moto)

Wengi mnapambana na wachawi tuu kila siku, unapiga wachawi wa2 wa3 hapo mtaani na hawakomi, wanakusumbua kweli, kwani hao ni ma-agent tu, wanaopata msaada tokea kwenye anga, hewa, maji na ardhi. (Ni sawa na kuhangaika na kichuguu wakati huna habari na milima na majabali) jifunze sasa

° Mpinga Kristo Ufunuo 16:13 “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka (Lucifa), na katika kinywa cha yule mnyama (the beast), na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani;…”

Hapa ndipo yupo shetani mwenyewe, na nafsi zake, yaani miungu yote (Dagoni, Baali, Maashtorethi, Artemi, Kemoshi, Dragon nk) . Roho za Udanganyifu ndio Nabii wa Uongo wakitenda kazi pamoja na mnyama “The Beast” (Ufunuo 19:20) katika miujiza na ishara nyingi za udanganyifu…wengi wapo hapa Dar, na Loloindo, Nigeria, Korea & South Africa nk na kuwadanganya wengi wengi wengi. Tumeona pia jinsi shetani alivyojificha nafsi yake ndani ya Adamu wa Kwanza na BWANA akamfunua na kumuangamiza.

° Mamlaka Kutoka 5:6-9 “Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao akisema …Wapeni watu hao kazi nzito zaidi, waitaabikie…” , Yeremia 50:17 “Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali, kwanza mfalme wa Ashuru amemla, mwisho Nebukadreza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.”  Matendo 12:1-2 “Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamwua Yakobo, na ndugu yake Yohana, kwa upanga

Umejionea jinsi falme & mamlaka wanavyojipanga ili kutaabisha kanisa, kulitawanya likose umoja, kuwafukuza, kuwala nyama, kuwavunja nguvu, kuwatenda mabaya, kuwaua kwa upanga, ajali nk. Tena sasa upo ufalme FEKI uliofunuliwa kwenye Ufunuo 17:9- “Hapo ndipo penye akili zenye hekima, … wafalme watano wamekwisha anguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado”  hawa ndio wenye ibada za wafu, kufukiza uvumba, kuzika wafu ndani ya masinagogi na kuwatukuza, waliomsulubisha YESU.

° Wakuu wa Anga/ Giza Isaya 14:12 “…Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyoya ya alfajiri, mwana wa asubuhi…”, 1 Famle 10:1 “Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Suleimani…” (ndiye Malkia wa Kusini) , Ufunuo 17:1-6 “…Njoo huku nitakuonyesha hukumu juu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi, ambaye wafalme wa nchi wamezini naye,…wamelevywa kwa mvinyo wa uasherati wake,…na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba na Machukizo ya nchi…”  ndio shina la uzinzi, dhuluma, starehe, ulevi,ufisadi n.k.

° Mapepo, soma Ufunuo 12:7-8, soma Ufunuo 9:2-11 “…Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake…Abadoni, …na Apolioni  pia soma na Luka 10:19 “…Nyoka na nge…”
Pia ufahamu kuwa uchawi, uganga, dua, majini, visomo, ibada za sanamu, ramli nk sio kitu ila ni upuuzi tu.

° Miji ya kipepo, 1 Samweli 6:17-18 inatuonyesha miji miTano ambayo ni ngome za Wafilisti hata leo…Gathi, Ekroni, Ashdodi, Gaza na Ashkeloni”  na Yeremia 50:24 “Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa…ukakamatwa kwa sababu ulishindana na BWANA  na Ufunuo 18:2 “…Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho chafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza” Katika vita jifunze ni wapi wanapata nguvu na ni wapi wanajificha.

HITIMISHO:
Maombi tuombayo hapa ndio ya ki-mamlaka katika KUMILIKI juu ya nchi, sawasawa na NENO la BWANA Ufunuo 5:10 “…Ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Tena imeandikwa Ufunuo 20:1-6 “… bali watakuwa makuhani wa Mungu, na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu




Tunatawala kwa NENO la BWANA, tena kwa ujasiri mkubwa, maana tunatembea na BWANA, na kupigana na MKONO WA BWANA wenge nguvu na uweza mkuu. Haijalishi ni maadui gani , wapo wapi, au wana silaga gani, wametoa kafara ipi, wanaongozwa na miungu ipi, wamejificha mahali gani…yote hiyo sio kitu mbwlw za BWANA maana Zaburi 89:1-52 “Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA? … Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu…BWANA, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU?...Mkono wako ni mkono wenye uweza, Mkono wako una nguvu, Mkono wako wa kuume umetukuka…Na ahimidiwe BWANA milele, Amina na Amina”. Je umeuona UTIISHO huo ?


Sasa basi, ni lazima utembee katika nguzo NNE za kanisa ili kupata HAKIKA ya ushindi;
◊ NENO : Lazima uwe na hazina kubwa ya NENO moyoni mwako, ufahamu ni NENO gani litumike kwa wakati gani na kwa kusudi gani. Nguvu ndani ya NENO + Hakika juu ya NENO =  Huachilia nguvu kubwa ya KiUngu katika KUTAWALA. Waebrania 4:12 Maana NENO la Mungu li HAI, tena lina nguvu…”.

◊ IMANI : Hapa hakuna mjadala, maana alichokisema BWANA ndio kitakachosimama , hivyo chochote utamkacho kwa NENO la BWANA na kwa Jina la Yesu, hakika yake kimefanyika. Kwa maana ukitamka Ufunuo 18:2 imekuwa, ukitamka Hesabu 23:23 imekuwa, kila utamkacho kitafanyika kwa JINA LA YESU.
◊ UTII : Msikilize Roho Mtakatifu akuongoze kila uombapo, usienende kwa mazoea au kwa akili zako. Tumepewa Roho 7 za Mungu zinazotenda kazi ndani ya kaniza Isaya 11:2-3 Roho ya hekima, ufahamu, shauri, uweza, maarifa, nguvu na kumcha BWANA. 1 Samweli 30:8Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata, kwa kuwa hakika utawapata…”

Hapo ni wazi Daudi aliomba kwa Roho wa Shauri , na akatenda kwa UTII. Usienende kwa akili zako.

◊ UTAKATIFU : Zaburi 16:3 Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, Hao ndio nipendezwao nao” imeandikwa Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema,…” imeandikwa Yohana 14:23 …Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda” .
Utakatifu ndio kulishika, kulitunza na kulitenda NENO la BWANA, kunakopelekea Mungu kukupenda na kufanya kazi pamoja nawe, na kujidhihirisha kwako.

Maombi ya KUTAWALA majibu yake ni papo kwa hapo, wala usisubiri ishara, kwa maana HAKIKA yake yametimia. Unatakiwa kabla kuomba kwanza muulize BWANA, je vita unavyoenda kupigana vinabeba utukufu wa Jina la BWANA? Je unaomba ki-mazoea au Roho amekushuhudia ?. Majira ya sasa kuna siri nyingi sana zinazofunuliwa kwa kanisa kupitia Roho Mtakatifu.
Unapopigana vita vya rohoni, hakikisha umepiga na kuharibu kabisa maeneo haya ya adui;

□ Madhabahu zao           □ Ibada zao                         □ Kafara zao                       □ Sadaka zao
□ Maagano yao □ Kiapo chao                      □ Siri zao                              □ Nguvu zao
□ Uweza wao                    □ Mamlaka yao □ Maarifa yao                    □ Hekima zao
□ Silaha zao                        □ Mavazi yao                     □ Maumbo yao □ Milki zao
□ Mahali pao                      □ Maficho yao                   □ Minara zao                      □ Nguzo zao
□ Sauti zao                          □ Lugha zao                        □ Utendaji wao □ Ramani zao
□ Kuona kwao                   □ Farasi zao                        □ Magari yao                      □ Mawasiliano yao
□ Masaidiano yao            □ Tumaini lao                     □ Mashtaka yao                □ Pembe/Pete/Fimbo zao
□ Vituo vyao vya ku-recharge nguvu (bahari,maziwa,makaburi,
milima,nyota,ishara,masinagogi nk)
Roho wa Maarifa atazidi kukufundisha na kuachilia kwako mambo mapya kila ujinyenyekeshapo kwa BWANA. Umenisikia, narudia kusema “kila ujinyenyekeshapo mbele za BWANA ndipo utakapopewa mafunuo mapya

Kwa NENO hili 2 Samweli 8:14 “…naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.”  Mungu wa Eliyah, Mungu wa Daudi, Yeye aliye HAI na akupe kushinda kila usimamapo na kupigana vita katika kusudi la BWANA kwa UTUKUFU wa Jina lake. AMINA na AMINA.


MWISHO WA SOMO. Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka na Mungu wa Eliyah akubariki sana. Amina.

Jipime tu, mwezi wa juzi wote, siku kwa siku, ULIOMBA nini, Jitathmini, mwezi jana wote, siku kwa siku, uliomba nini…. je una udhihirisho gani wa yale uliyoyaomba muda wote huo? Na mwezi huu wa sasa je , unaomba jambo gani ? FANYA TATHMINI YAKO BINAFSI, pia tazama wapi kanisa lilipo, na wewe ulipo ?

Hivyo basi; Tumejifunza MAENEO MA-NNE KATIKA MAOMBI, na tumeona ni vema kujipanga katika kila ENEO moja moja na kuomba kwa mzigo kwa NENO la BWANA ili kupokea udhihirisho wa kile tuombacho. Tumeona si vema kuchanganya changanya maombi na usikumbuke wala kupokea ulichoomba. Roho wa BWANA akupe kujifunza na kupokea kile ulichoandaliwa na BWANA kupitia mafundisho haya. AMEN.

*** BONUS ***

Angalizo la awali: Udhihirisho wa maombi unategemea MTAWALA na MAJIRA anayotawala…

Imeandikwa Mwanzo 1:16-18 16’ “Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku…18’ na kuutawala mchana na usiku, na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema”   

Kutawala ni mamlaka aliyonayo mtawala na majira ya kutawala, wakati “mchana & usiku” ndio majira na nyakati za kutawala, kila mmoja Jua & Mwezi kwa nafasi yake sawasawa na agizo la BWANA.

Sasa natakufundisha (kwa kifupi) habari ya miaka 1,000 (majira) ya kanisa kutawala pamoja na BWANA, na kuhusu Adamu wa Pili (mtawala) , kinyume na Adamu wa Kwanza. “Adamu wa Kwanza” alikuwa na nafsi ya UASI, ndio nafsi ya shetani, ya giza, ya ukiwa. Hivyo ni lazima ujue miaka elfu moja ya mwisho na Adamu wa Pili, aliyetoka mbinguni.
» Imeandikwa, Ufunuo 20:1-6 “… bali watakuwa makuhani wa Mungu, na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu Sasa (as you read), majira hii kanisa lipo mahali pa JUU sana, ndani ya miaka 1,000 ambayo BWANA anatawala pamoja na kanisa. Ni lazima, kila uombapo, ufahamu wako uwe ndani ya miaka 1,000 ya kanisa kutawala. Ni lazima pasi ipate moto wa kutosha ndipo uweze kunyoosha nguo, si vinginevyo. Ni lazima maji yachemke vya kutosha ili kupata maji ya chai, si vinginevyo. Ni lazima ujue majira sahihi ya utawala ili utamkapo katika kuomba uwe na udhihirisho. Hivyo basi fahamu kuwa “sasa” tupo ndani ya miaka elfu moja ili tupokee udhihirisho;  maana awali bado ‘kerubi muasi’ yaani mauti, giza na dhambi vilikuwa bado vinatawala na kupambana na kanisa 1 Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti” ambapo sasa mauti ameshaangamizwa, hana nguvu 1 Wakorintho 15:54-55 kanisa lina mamlaka juu ya mauti na ufalme wote wa giza na kuzimu.
Narudia, fahamu tupo majira ya miaka elfu ya kanisa kutawala pamoja na Kristo. Jipatanishe na majira hiyo kila uombapo, maana pasipo hivyo utaomba majira za miungu ya sanamu.

» Imeandikwa, Warumi 5:17 “Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa , yule mmoja, Yesu Kristo.”

Umesoma Warumi 5:17 kuwa dhambi alitawala (sasa nguvu ya dhambi imeangamizwa), lakini baadae (sasa) waliookoka ndio wanatawala katika Kristo; kwa maana Adamu wa Kwanza alibeba umauti, na Adamu wa Pili ndie Yesu Kristo amebeba uzima. 1 Wakorintho 15:22 “Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika katika Kristo wote watahuishwa” Umeona Adamu wa Kwanza ana umauti kwa wote, na Adamu wa Pili ndie Kristo amebeba roho ya kuhuisha . Imeandikwa ….
 1 Wakorintho 15:45-47 “Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni

No comments:

Post a Comment