Thursday, May 30, 2019

Kwa nini Mungu ali-Muumba mwanadamu?


by William Meja

i.                     Ili kuwa na ushiik na Mungu – Johana 4:24,Deut 4:24.
ii.                   Kudhihirisha asili yake – zaburi 82:6(kimwili sisi ni watoto wa wanadamu lakini kiroho sis ni watoto wa Mungu.)- waefeso 3:10-11.

Friday, October 21, 2016

UNYENYEKEVU



  • Yohana 12:32 - Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
  • 1 Wakorintho 1:17 - Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
  • 1 Wakorintho 1:27-29 - Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
  • 1 Wakorintho 2:4 - Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

USINGIZI MZURI



  • Ayubu 11:18, 19 - Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama. Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako.
  • Zaburi 3:5 - Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.
  • Zaburi 4:8 - Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
  • Zaburi 91:5 - Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
  • Mithali 3:24 -Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.

KUDAI NCHI



  • Mwanzo 13:17 - Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
  • Mambo ya Walawi 25:23 - Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu.
  • Kumbukumbu la Torati 11:24A - Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.
  • 2 Samweli 22:20 - Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
  • Zaburi 2:8 - Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
  • Zaburi 107:6, 7 - Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.
  • Isaya 30:21 - Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
  • Mathayo 7 :7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
  • Waebrania 11:8 - Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
  • Mwanzo 28:15 - Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
  • Kutoka 23:20 - Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
  • Kutoka 32:34 - Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
  • Kutoka 33:14 - Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.
  • Kumbukumbu la Torati 28:6 - Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
  • Zaburi 105:13-15 - Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.

KUPAMBANA NA ADUI



Kupinga Ibilisi / Resisting The Devil
  • Isaya 59:19B - Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.
  • Mathayo 10:1 - Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
  • Mathayo 16:19 - Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
  • Marko 8:33B - Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
  • Luka 9:1 - Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

UPOTOSHAJI



  • Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. - Warumi 1:18-28