Friday, October 21, 2016

KUDAI NCHI



  • Mwanzo 13:17 - Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
  • Mambo ya Walawi 25:23 - Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu.
  • Kumbukumbu la Torati 11:24A - Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.
  • 2 Samweli 22:20 - Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
  • Zaburi 2:8 - Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
  • Zaburi 107:6, 7 - Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.
  • Isaya 30:21 - Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
  • Mathayo 7 :7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
  • Waebrania 11:8 - Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
  • Mwanzo 28:15 - Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
  • Kutoka 23:20 - Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
  • Kutoka 32:34 - Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
  • Kutoka 33:14 - Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.
  • Kumbukumbu la Torati 28:6 - Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
  • Zaburi 105:13-15 - Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.
  • Zaburi 107:28-30 - Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi yake yakanyamaza. Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia Naye huwaleta mpaka bandari waliyoitamani.
  • Zaburi 121:8 - Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
  • Zaburi 139:9, 10 - Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
  • Isaya 45:2, 3 - Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Ezekieli 11:16 - Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi, Ikiwa mimi nimewahamisha, wakae katika mataifa, na ikiwa mimi nimewatawanya katika nchi kadha wa kadha, pamoja na hayo nitakuwa patakatifu kwao kwa muda mchache, katika nchi zile

No comments:

Post a Comment