Friday, October 21, 2016

SIFA



2 Mambo ya Nyakati 20:22 - Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.
  • Nehemia 8:10B - Kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
  • Zaburi 50:23 - Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
  • Zaburi 89:15 - Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako.
  • Yeremia 30:19 - Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.
  • Matendo ya Mitume 2:47 - Wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
  • Wafilipi 4:6 - Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
  • Mathayo 5:10-12 - Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
  • Luka 6:22, 23 - Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
  • Yohana 16:33 - Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
  • Matendo ya Mitume 5:41 - Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo.
  • Warumi 9: 20 - La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
  • 2 Wakorintho 6:10 - Kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
  • Wafilipi4:11B  -Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.
  • 1 Wathesalonike 5:18 - Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
  • Waebrania 10:34 - Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
  • 1 Petro 1:8 - Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
  • 1 Petro 3:14 - Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
  • 1 Petro 4:13, 16 - Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.

Kumsifu na kumshukuru Bwana / Praising and Thanking the Lord


  • Zaburi 32:11 - Mfurahieni Bwana; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
  • Zaburi 33:1 - Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
  • Zaburi 34:1 - Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
  • Zaburi 35:28 - Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
  • Zaburi 68:19 - Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu.
  • Zaburi 71:8 - Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.
  • Zaburi 92:1, 2 - Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku.
  • Zaburi 100:4 - Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
  • Zaburi 103:1, 2 - Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
  • Zaburi 107:8 - Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
  • Zaburi 107:22 - Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.
  • Zaburi 113:3 - Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
  • Maombolezo 3:41 - Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni Mioyo yetu na mikono.
  • Yona 2:9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.
  • Waefeso 5:19, 20 - Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
  • 1 Wathesalonike 5:18 - Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
  • Waebrania 13:15 - Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
Ufunuo WA Yohana 19:5B - Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu

No comments:

Post a Comment