MIMBA NA UZAZI
- Mwanzo
49:25 - Naam, kwa Mungu wa baba yako
atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi
vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.
- Kutoka
1:7 - Na wana wa Israeli walikuwa na
uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na
kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
- Kumbukumbu
la Torati 7:13A, 14A - Naye
atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo
lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako,
maongeo ya ng'ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia
baba zako kuwa atakupa. Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu
mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.
- Ayubu
31:15 - Je! Huyo aliyenifanya mimi
ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga
tumboni?
- Zaburi
112:2 - Wazao wake watakuwa hodari
duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
- Zaburi
113:9 Huweka nyumbani mwanamke aliye
tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.
- Zaburi
127:3 -Tazama, wana ndio urithi wa
Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.
- Zaburi
139:13 - Maana Wewe ndiwe uliyeniumba
mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
- Zaburi
147:13 - Maana ameyakaza mapingo ya
malango yako, Amewabariki wanao ndani yako.
- Isaya
40:11 - Atalilisha kundi lake kama
mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani
mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
- Isaya
44:3, 4 - Kwa maana nitamimina maji juu
yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho
yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; nao
watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.
- Yeremia
1:5 - Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii
wa mataifa.
- Luka
1:45 - Naye heri aliyesadiki; kwa
maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
- Waebrania
11:11 - Kwa imani hata Sara mwenyewe
alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa
alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
- Zaburi
18:19 - Akanitoa akanipeleka panapo
nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
- Zaburi
31:2 - Unitegee sikio lako, uniokoe
hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
- Zaburi
34:7 - Malaika wa Bwana hufanya
kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
- Zaburi
40:13 - Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa,
Ee Bwana, unisaidie hima.
- Zaburi
40:17 - Nami ni maskini na mhitaji,
Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu,
usikawie.
- Zaburi
50:15 - Ukaniite siku ya mateso;
Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
- Zaburi
61:2 - Toka mwisho wa nchi
nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
- Zaburi
91:14 - Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
- Mithali
11:21B - Bali wazao wa wenye haki
wataokoka.
- Isaya
40:29-31 - Huwapa nguvu wazimiao,
humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na
kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata
nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala
hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
- Isaya
65:23 - Hawatajitaabisha kwa kazi
bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao
waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.
- Isaya
66:7, 9 - Kabla hajaona utungu alizaa;
Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume. Je! Mimi nilete
wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana; mimi nizalishaye, je!
Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
- Yohana
16:21 - Mwanamke azaapo, yuna huzuni
kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile
dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.
- 1
Wakorintho10:13 - Jaribu
halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni
mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na
lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
- 2
Wakorintho 12:9 - Naye
akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika
udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa
Kristo ukae juu yangu.
- Wagalatia
6:9 - Tena tusichoke katika kutenda
mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
- Wafilipi
4:13 - Nayaweza mambo yote katika
yeye anitiaye nguvu.
1 Timotheo 2 :15 - Walakini
ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso,
pamoja na moyo wa kiasi
No comments:
Post a Comment