“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”
Katika
kizazi chetu, tunashuhudia waganga wa kienyeji wakipata umaarufu wa
kupata wateja wengi, na moja ya tiba wanayotoa ni KUSAFISHA NYOTA, hii
ina manisha kuondoa Mikosi, Nuksi n.k.
Dada
mmoja alitoa ushuhuda wa mambo aliyofanyiwa na Fundi (Mganga wa
Kienyeji) alipoenda kusafisha nyota ya Mapenzi – Tatizo lake lilikuwa
kila akimpata Mwanaume anaishia kumtimizia haja ya Mwili baadaye
anaachwa. Katika tiba ya kusafisha Nyota alifanyiwa Mambo ya aibu,
ikiwemo kuchanjwa chale sehemu zake za Siri na kulazimika kufanya Ngono
na huyo fundi ikiwa ni sehemu ya Tiba. Pamoja na yote hayo hakufanikiwa,
mpaka alipojisalimisha Kwa Mungu. Hadi sasa baada ya maombi, Yule Dada
ana Mume na watoto Ndani ya YESU.
Vijana
wengi, wanahangaika kwa kukosa elimu ya Mungu, wanajiingiza katika
mitindo ya maisha inayowatenga na Mungu wao, na mwishowe wanaishia
kukata tamaa. Leo Baadhi ya Maswali yanayoulizwa sana na
Vijana
Swali: Je ni halali kuwa na wachumba zaidi ya Mmoja?
Jibu: Hapa
kuna shida, huenda hata maana ya uchumba haieleweki, mchumba ni Yule
ambaye tayari mmekubaliana na amekubalika na wazazi. Mahusiano mengine
nje ya hayo sio uchumba. Mchumba ni mmoja tu, ni udanganyifu kuwa na
wachumba wengi. Ukimtegemea Mungu atakupatia Mmoja anayefaa, kuliko
kujiingiza katika mtego wa kumkubali kila anayeonekana, mwisho ya yote
ni kujichanganya na wote kutoweka.
Swali: Nina Mchumba anataka TENDO la Ndoa kwanza kabla ya kuoana.
Jibu:
Kama neno lilivyo, TENDO la NDOA ni kwa walio oana tu, ndiyo maana
hakuna TENDO la UCHUMBA. Kitendo hicho nje ya Ndoa ni UZINIFU. Na Amri
ya saba inasema “USIZINI” Kutoka 20:14. Athari za kufanya Ngono kabla ya
Ndoa ni nyingi sana, Siku zijazo nitakuwa na mada hiyo tu. Matatizo
katika ndoa za siku hizi asilimia kubwa yanatokana na Tendo la Ngono
kabla ya Ndoa.
Swali: Muda unaenda Siolewi! Nifanyeje?
Jibu:
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mabinti wasiolewe, zikiwemo maisha
aliyoyapitia huko Nyuma, kukataa wachumba katika muda muafaka n.k.
pamoja na sababu zozote zile – Ukimtemea Mungu 100%, ninakuhakikishia
kuwa Utaolewa. Jumapili ijayo tunapokea mahali ya Dada mwenye Umri wa
Miaka 47 anaolewa na mwanaume wa miaka 48. Wote hawajawahi kuoa au
kuolewa. Huwezi amini, lakini ndivyo. KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA, BILA
KUJALI YA NYUMA, TOA MAISHA YAKO KWA MUNGU NAYE ATAJIBU KWA WAKATI.
Swali: Sioni mwanamke wa Kuoa, nifanyeje?
Jibu:
Wanawake wapo, ila huwaoni kwa sababu unatumia vipimo vya kibinadamu.
Mwambie Mungu atakuletea Mwenzi wa kukufaa kwa Vipimo vya Mbinguni.
Tatizo kubwa, Vijana wa kiume wanatawaliwa na TAMAA za ngono, hivyo wana
ONJA ONJA na mwishowe wanaona wanawake wote walishaonjwa. Jambo la
kushangaza ni hili – Wanadai mabinti sio waaminifu wakati wao wenyewe
ndiyo wamewafikisha katika hali hiyo. Inakuwaje Mtu asiyemwaminifu
anatafuta kuishi ni Mtu Mwaminifu? Huko ni kujichanganya.
No comments:
Post a Comment