Friday, October 21, 2016

UAMINIFU



  • Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; - Wakolosai 3:9
  • Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. - Warumi 12:17
  • Tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu. -    II Wakorintho 8:21
  • Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. - Mithali 11:1,3
  • Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila. -   Mithali 12:13,17
  • Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. - Mithali 28:13
  • Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. -
    Yakobo 5:16
  • lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. - II Wakorintho 4:2

No comments:

Post a Comment