Wednesday, October 12, 2016

MWONGOZO WA KIBIBLIA KUHUSU KUPUMZIKA KWA BWANA



  • Kutoka 33:14 -Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.
  • 1 Samweli 9:27 -Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.
  • 2 Mambo ya Nyakati 14:7B -Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta Bwana, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa.
  • Zaburi 4:4 - Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
  • Zaburi 27:14 -Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
  • Zaburi 37:7 -Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.
  • Zaburi 40:1 -Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
  • Zaburi 46:10A -Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
  • Zaburi 55:22 -Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
  • Zaburi 62:8 - Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
  • Isaya 26:3 -Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
  • Isaya 30:15B -Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
  • Isaya 32:17 -Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
  • Isaya 40:31 -Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
  • Yeremia 17:7 - Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
  • Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
  • Maombolezo 3 :25, 26 -Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu.
  • Mathayo 11:28-30 -Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
  • Wafilipi 4:7 -Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
  • 2 Timotheo 1:12B -Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.
  • 1 Petro 5 :7 -Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

No comments:

Post a Comment