- Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. - 1 Timotheo 6:10
- Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. - Mathayo 6:33
- Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. - Malaki 3:8-10
- Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. - Wafilipi 4:19
- Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. - Zaburi 37:25
- Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. - 1 Yohana 5:14,15
- Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. - Zaburi 23:1
- Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema. - Zaburi 34:10
- Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. - Zaburi 68:19
- Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. - Zaburi 81:10b
- Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. - Zaburi 84:11b
- Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. - Zaburi 145:15b,16
- Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa. - Mithali 13:25
- Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; - Isaya 1:19
- Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka. - Ezekieli 34:26
- Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. - Mathayo 6:8b
- Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. - Mathayo 7:7,8
- Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? - Mathayo 7:11
- Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. - Mathayo 21:22
- Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La! - Luka 22:35
- Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. - I Wakorintho - 9:14
- na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. - Yohana 3:22
Wednesday, October 12, 2016
MWONGOZO WA BIBLIA KUHUSU UCHUMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment