Friday, October 21, 2016

FURAHA




  • Zaburi 5:11 - Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
  • Zaburi 16:11 - Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
  • Zaburi 30:5 - Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
  • Zaburi 126:5 - Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
  • Zaburi 128:1, 2 - Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
  • Isaya 35:10 - Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
  • Yohana 15:11 - Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.
  • Warumi 14:17 - Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

No comments:

Post a Comment