Monday, May 12, 2014

SOMO LA LEO JUMAPILI

FANS WOTE WA BLOG HII SIKU YA LEO JUMAPILI 11/05/2015. ILIKUWA NI SIKU YA PEKEE SANA.
NENO KUU:  MJUE SANA BWANA MUNGU WAKO UWE NA AMANI.
NENO KUU: AYUBU 22:21.

MAHUBIRI: Ni kweli kwamba hakuna maisha bila ya kuwa na bwana Mungu japo watu tunajitia MOYO. Lakini ukweli ndoo hivo. Muhubiri alisema Kumjua Mungu kunapimwa kwa matatizo, je unapopata tatizo unachukuaje hatua, Naomba na wewe ujitadhimini katika Maisha yako.
Mtu anayemjua Mungu akuna kitu cha kuweza kumtenga yeye na bwana Mungu wake. Yeye mambo yote kwake ni Mazuri anafuraha wakati wote awe na pesa asiwe nazo yote sawa anasonga mbele na yesu.

Lakini pia akazungumzia suala la Maisha akasema Mtu anayemjua sana mungu, Kwanza atabarikiwa kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Kumbukumbu 28:1-14. Pili  mtu anayemjua Mungu atafuti watu wakumtia moyo, Anajitia Moyo yeye mwenyewe, Anakuwa na bidii, Anakuwa mwenye kufanya mashauri Mengi, isitoshe anasoma neno na kufanya Maombi.
 Hakuishia hapo akazungumzia Kuhusu Suala la Ndoa, Hukimjua Mungu wewe kama ni Mwanaume Utajua Kupenda na kama ni Mwanamke Utajua Jinsi ya Kutii. Na akuta kuwepo na MCHECHETO. so lazima tumwombe sana Mungu atupe Kumjua tusijione tumefika.

Mwisho kabla ya maombezi alizungumzia kuhusu baadhi ya watu waliopata kumjua Mungu wakina Shedrack, Meshack na Ebednego walivyo kataa kula chakula cha Mfalme na wakatupwa kwenye tanuru la Moto lakini hawakukata tamaa. lakini pia akawazungumzia wakina Musa, Ayubu, Daudi,Paulo, Yusuph n.k
(JE WAJUA KIZUIZI CHA MEMA YAKO? YEREMIA 5:25).
WATUMISHI WAKIPIGA MAOMBI KUMPINGA SHETANI ASIPATE NAFASI.

WANAKWAYA WAKIWA STAGE WANATUMBUIZA WAKATI WA IBADA JUMAPILI YA LEO TAREHE 11/05/2014.

No comments:

Post a Comment