FANS HIZI NDIZO SALA AMBAZO MIMI UPENDA KUZITUMIA KILA SIKU NIMEONA NI VYEMA NA WEWE UPATE KUZITUMIA.
WAEB 1:15-19.
SALA YA ASUBUHI
Nakushukuru, Ewe Baba yangu wambinguni, kwa Jina la Mwana wako mpendwa Yesu Kristo kwa Kuwa umenilinda usiku huu na kunizuilia maumivu na hatari zote. Nakuomba, unilinde hata mchana huu wa leo, nisikose njia yako wala kupatwa na maovu. Unipe kukupemdeza na matendo yangu, mwenendo wangu uwe mzuri. Kwa mwili wangu na moyo na vyote nilivyo navyo naviweka mkononi mwako. Malaika wako mtakatifu awe pamoja nami, shetani asinishinde Amen.
SALA YA JIONI.
Bwana Mungu, Baba yetu uliye mbinguni, uliyetulinda vema mchana huu, twakusihi utusamehe kwa yale yote tuliyoyakosa, utungazie nuru ya huruma zako, sisi tulale tukiwa na msamaha wako, tutulie na kustarehe usiku huu, Wewe utulinde, utuamshe wenye nguvu; kwa yesu kristo, Mwana wako na Bwana wetu. Amen
No comments:
Post a Comment